Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2017

Vitu vitatu muhimu katika mahusiano

Natumai hu mzima wa afya mpendwa wangu msomaji. Kwanza kabisa Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuweza kushirikishana na wewe mambo kadhaa ambayo wengi wamekuwa wakipata shida sana katika kuyakabili ndani ya maisha yao. Wapo wengi walio katika mahusiano na wenzi wao ila kumekuwa na matatizo ya hapa na pale ambayo husababisha aidha kuvunjika au ugomi wa kila siku ndani ya mahusiano. fuatana nami...... 1. UAMINIFU Moja kati ya kitu cha msingi sana sana katika mahusiano yoyote yale ni uaminifu. Najua unaweza ukawa shahidi wa hili ninalosema, mahusiano ya wengi leo yameekosa uaminifu na kama upo basi ni kwa asilimia chache sana. Nikweli hutakiwi kumwamini mtu kwa asilimia mia moja lakini wengi wetu tuna asilimia  ishirini chini ya mia jambo ambaloni tatizo.